Back to top

Binti akatwa mkono kwa madai ya kumkataa aliyemposa Uganda.

27 July 2020
Share

Binti wa miaka 16 nchini Uganda amekatwa mkono  baada ya kukataa kuolewa,tukio hilo linadaiwa kutekelezwa na mwanaume ambaye amemkataa.

Polisi nchini humo wanaendelea kuchunguza tukio hilo la binti huyo wa kidato cha pili ambaye pia amejeruhiwa katika maeneo mengine ya mwili.

Kutokana na maelezo ya Binti huyo amesema mwanaume huyo alitaka kumuoa lakini alikataa kwa sababu anapenda masomo yake hivyo jibu alilolitoa halikumfurahisha.