Back to top

BOMBA EACOP LACHEPUSHWA KUHESHIMU MILA

23 March 2023
Share

Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), imekubaliana na Jamii ya kabila la Wataturu iliyopo wilayani Igunga mkoani Tabora, kuchepusha mradi huo, ili usipite kwenye eneo la makaburi ya wazee maarufu, kwa ajili ya kulinda mila na desturi za kabila hilo, huku jamii hiyo ikidai kuwa endapo mradi huo utapita kwenye eneo hilo inaweza kusababisha majanga katika familia husika ikiwemo laana na vifo.