Back to top

Daraja la pili kwa urefu kanda ya Afrika mashariki lazinduliwa Uganda.

18 October 2018
Share

Uganda imezindua rasmi daraja lenye urefu wa mita 525 linalopita juu ya mto Nile, likiwa refu zaidi nchini humo linalounganisha sehemu ya mashariki na sehemu kubwa ya Magharibi mwa Uganda.

Daraja hilo ni la pili kwa urefu baada ya lile la Kigamboni lililopo nchini Tanzania kanda ya Afrika Mashariki kukamilika kwake kumefadhiliwa na serikali ya Japan kwa asilimia 80, huku Uganda ikichangia asilimia 20 tu.

Waziri wa maswala ya nje wa Japan Masahisa Sato,ametaja ufadhili huo kama thibitisho la urafiki wa dhati kati ya mataifa hayo mawili.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameishukuru serikali ya Japan kwa mchango wake wa kuchochea maendeleo ndani ya taifa lake.

Daraja hilo lenye njia 4 litatumiwa na waendeshaji magari na wanaotembea kwa mguu pekee huku zee la Nalubaale likitumiwa na wahudumu wa boda boda na baiskeli.

"Daraja hili ni kwa wanaoendesha magari na wanaoenda kwa mguu, wa piki piki msijaribu kukanyaga hapa" Amesema Museveni

Daraja hilo ni la umuhimu Mkubwa kwa mataifa ya ndani na nje ya kanda ya Afrika mashariki yanaotegemea bandari ya Mombasa.