Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ukusanyaji wa mapato ya maegesho katika eneo la Ifunda wilayani Iringa na kuwasilisha taarifa kamili kuhusu namna mapato hayo yalivyokuwa yakikusanywa kabla na baada ya mabadiliko ya mfumo wa ukusanyaji pamoja na matumizi yake.

