Back to top

DC MSAFIRI AAGIZA KUBANWA MTENDAJI WA KIJIJI RUVU ALIYEJICHOTEA FEDHA

27 May 2022
Share

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Bi.Sara Msafiri, ameagiza Mtendaji wa Kijiji Cha Ruvu Stesheni Neema Shanga ambaye kwa sasa kahamishwa kituo cha kazi kufuatia tuhuma zinazodaiwa kujichotea fedha za Kijiji kinyume na taratibu kiasi cha sh.650,000 azirejeshe Mara moja.

Ameeleza hayo alipofika katika kijiji cha Ruvu Station kilichopo Kibaha vijijini Mkoa wa Pwani kuhusiana na kero zinazowakabili ikiwemo kutofanyika mkutano wa kijiji hasa mapato na matumizi pamoja na ujenzi wa Zahanati.