Back to top

DKT.MABULA ATAKA MAFUNZO YA MAADILI KWA MADALALI

30 January 2023
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula, ameataka kutolewa mafunzo ya maadili kwa Mawakala wa Mali Zisizohamishika (MADALALI)

Amesema, pamoja na mafunzo yanayotolewa kuwa ya kitaalamu zaidi lakini upo umuhimu mkubwa wa kutolewa, mafunzo yanayohusu maadili kwa kuwa eneo hilo limekuwa likisababisha malalamiko mengi kwa jamii.

Dkt.Mabula amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya muda mfupi ya Mawakala wa Mali zisizohamishika (MADALALI) yanayoendeshwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kushirikiana na Chama cha Mawakala wa Mali Zisizohamishika (AREA) yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Ametolea mfano wa Mawakala kuchukua kamisheni toka pande zote zinazohusika kwenye mauziano au upangaji nyumba na kubainisha kuwa suala hilo limekuwa kichocheo cha kupanda bei au kodi za nyumba na kuzidi viwango vya soko lengo likiwa kujipatia kamisheni kubwa na hivyo kuvuruga mwenendo wa soko la milki nchini.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, wapo Madalali wanaolalamikiwa kufanya vitendo vya utapeli ambapo huwadanganya wateja na kusababisha wateja hao kununua viwanja huku wakijua fika kuwa viwanja hivyo ni mali ya watu wengine  na mwisho wa siku hujipatia fedha isivyo halali.