Back to top

ELIMU YA MONTESSORI YAPIGIWA CHAPUO

12 June 2023
Share

Kamishna wa Elimu Tanzania, Dkt.Lyabwene Mtahabwa, amesema elimu inayotolewa na Jumuiya ya Montessori hapa nchini inamanufaa kwa jamii kwani imejikita katika kuwaelimisha watoto katika umri mdogo.

Dkt.Mtahabwa amesema hayo mkoani Dar es Salaam nakueleza kuwa Jumuiya hiyo inafanya kazi kubwa katika kutoa elimu kwa watoto wa kitanzania na kwamba umefika wakati elimu hiyo imepewe kipaumbele

Kamishna huyo wa elimu amesema ni jukumu la Jumuiya hiyo ya Montessori amesema ni kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa kuwakaribu na watoto wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya Montessori Sarah Kiteleja amesema Mazingira ya Montessori yanamwandaa mtoto tangu anapozaliwa hadi umri wa miaka 6 na wanalindwa na kupata elimu bora.