Back to top

Faini za wakwepa kodi zanunua mabati ya kujengea madarasa Mbeya.

15 January 2019
Share

Zaidi ya shilingi milioni 74 ambazo zimetokana na faini za makosa mbalimbali ya ukwepaji kodi mkoani Mbeya zimetumika kununua mabati kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwezesha wanafunzi zaidi ya wanafunzi 6000 ambao wamekwama kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu waanze masomo.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema mkoa mzima wa Mbeya unahitaji vyumba vya madarasa 143 ili watoto wote 6,225 ambao hawajaanza masomo waweze kwenda shuleni ambapo wananchi wenyewe wameanza  kujenga kwa nguvu zao na sasa serikali ya mkoa imeamua kuwaunga mkono kwa kutoa mabati hayo pamoja na kufanya maandalizi ya upatikanaji wa madawati.