
Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 8.75, kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vipya 15, na kukamilisha vituo vingine vitano katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya serikali ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Hayo yamesemwa Bungeni na Naibu Waziri TAMISEMI Mh Deogratius Ndejembi, akijibu swali kuhusu nini mpango wa serikali katika kujenga na kukarabati vituo vya afya, ili kutoa huduma bora ikiwemo kwa wenye bima ya afya, ambapo amesema utekelezaji huo ni mpango na mikakati Madhubuti ya serikali ya kujenga na kukarabati vituo vya afya nchini
Amesema vituo hivyo pamoja na majukumu mengine vitapaswa kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) pamoja na mfuko wa afya wa jamii (iCHF)
Pamoja na hayo Mh Ndejembi, amesema katika mwaka wa fedha wa 2021/22 jumla ya shilingi bilioni 118, zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 236 katika Kata za Kimkakati nchini.
