Back to top

GACHAGUA ADAI KSH. BIL. 16 ZILIIBIWA UTAWALA ULIOPITA

05 March 2023
Share

Makamu wa Rais nchini Kenya, Rigathi Gachagua amesema maafisa wa utawala uliopita waliiba shilingi Ksh.bil.16, katika kipindi cha kukabidhiwa kwa utawala kwa Rais wa sasa wa nchi hiyo, Dkt.William Ruto huku akibainisha kuwa pesa hizo zilikuwa zikisafirishwa kwenye makasha hadi uwanja wa ndege wa Wilson Jijini Nairobi hadi kwenye nyumba za watu fulani kwa kutumia helikopta.
.
Gachagua amesema hayo, kwenye mkutano na wataalamu kutoka Tetu, uliofanyika katika Kaunti ya Nyeri, ambapo amedokeza kuwa Ksh.bil. 10 ziliibiwa wakati wa kesi ya kupinga uchaguzi wa Rais, na Ksh.bil. 6 siku mbili kabla ya uchaguzi huku akimtuhumu Waziri wa Usalama wa Ndani katika utawala wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta Fred Matiangi kuhusika na wizi huo.