Back to top

HADI MACHI 2024, SERIKALI IMENUNUA MAGARI 796

16 April 2024
Share

Serikali imesema katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo zinafanyika na kufuatiliwa kwa ukaribu, hadi kufikia Machi 2024, ilikuwa imenunua jumla ya Magari 796, ambayo yamesambazwa katika Taasisi, Mikoa na Mamlaka za seriakli za Mitaa.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa TAMISEMI, Mhe.Mohamed Mchengerwa wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo.
.
Mchengerwa amesema kati ya Magari hayo, magari 316 yalikuwa kwa ajili ya kubebea wagonjwa (Ambulance), magari 212 kwa ajili ya usimamizi wa huduma za Afya za msingi, lishe na ustawi wa jamii katika Halmashauri 184 na Mikoa 26, magari 134 kwa ajili ya usimamizi na uratibu wa Shughuli za Elimu, magari 18 kwa ajili ya usimamizi wa miundombinu ya barabara inayosimamiwa na TARURA, magari 83 kwa ajili ya Viongozi wa Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa na magari 26 ni kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya Maendekeo katika ngazi ya mikoa.