Back to top

HAKUNA KIFO KIMETHIBITISHA KUWA NI UVIKO - UMMY

14 May 2023
Share

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, amesema mpaka sasa hakuna kifo kilichothibitisha kusababishwa na ugonjwa wa UVIKO-19 ambapo amewataka wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia hali hiyo.
.
Waziri Ummy amesema hayo, kupitia mtandao wake wa kijamii, kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea kupitia mitandao ya kijamii, juu ya kuibuka kwa ugonjwa wa UVIKO-19 nchini na kusababisha vifo.
.
Amesema kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki ya tarehe 6 - 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na ugonjwa huo, ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23.