
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amesema fremu za soko la Kariakoo hazijaanza kugawiwa, ambapo amewataka wananchi wa mkoa huo, kuepuka matapeli wanaowalaghai kuwa fremu za Soko hilo zimeanza kugawiwa.
.
Makalla ameyasema hayo, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa soko hilo ambalo hadi sasa ujenzi wa soko jipya umefikia 65% na ukarabati wa soko la zamani umefikia 85% huku akibainisha kuwa mradi ukikamilika utaratibu wa ugawaji utakuwa wazi kwa wananchi wote.
