
Wizara ya Fedha imesema kuwa haina mkopo wa Dola Bil. 4.1 (zaidi ya Shilingi trilion 10 za kitanzania) kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kama ambavyo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo imetoa onyo kwa wamiliki na watoa habari katika mitandao ya kijamii kuacha kutoa taarifa za upotoshaji na uzushi kwani ni kinyume sheria.

