Back to top

"HATUTATOA NAFASI KWA KIUMBE YOYOTE KUJA KUTUHARIBIA NCHI YETU"

19 May 2025
Share

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezielekeza Wizara zinazohusika pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoa ufafanuzi au kukanusha haraka matamko mbalimbali yenye nia ovu yanayotolewa na wanaharakati mbalimbali dhidi ya Tanzania.

Rais Samia amezungumza hayo katika uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la 2024) uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo Mei 19, 2025.

"Tumeanza kuona mwenendo wa wanaharakati wa ukanda wetu kuanza kuingilia na kuvamia mambo yetu, sasa kama kwao wamedhibitiwa, wasije kutuharibia huku" - amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema kuwa baadhi ya wanaharakati walishaharibu kwao, walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika, watu wako na amani, usalama na utulivu, ni hapa kwetu, hivyo tusitoe nafasi kwa kiumbe yoyote kuja kuharibu nchi yetu.