
Idadi kubwa ya watoto katika mikoa 7 nchini wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi ,kwa kukosa tiba za uhakika, ambapo baadhi yao wanaishi na Virusi Vya Ukimwi bila kupata dawa za kufubaza makali.
.
Hayo yamesemwa na Wadau wa Afya katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa Kushirikiana na Shirika la Misaada Kutoka Taifa La Marekani (USAID), wakati wakiweka mikakati ya kupunguza adha hiyo.
