Back to top

Idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu Tanga yaongezeka.

24 March 2019
Share

Idadi ya wagonjwa walioambukizwa Kifua Kikuu Mkoani Tanga inazidi kuongezeka kutoka 2,719 hadi kufikia 2,777 katika maeneo ya migodini hasa wilayani Korogwe.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kilele cha Siku ya Kifua Kikuu Duniani ambapo katika Mkoa wa Tanga yamefanyika katika viwanja vya Makinyumbi katika mji mdogo wa Hale, Wilayani Korogwe, Mratibu wa Kifua Kikuu Mkoa wa Tanga, Dkt.Raphael Mumba amesema hali ya maambukizi inaongezeka na inayoongoza ni wilaya ya Korogwe.

Katika maadhimisho hayo yaliyoambatana na kupima afya bure, Mratibu wa Kifua Kikuu Wilayani Korogwe, Dkt Baraka Mbwambo amesema katika kipindi cha mwaka huu wamekwenda katika mgodi wa Kalalani wilayani humu wamegundua idadi kubwa ya wagonjwa kufuatia kuunda vikundi- kazi ambavyo vinakwenda katika maeneo hayo na kukusanya makohozi.

Kufuatia hatua hiyo Mwakilishi Mkazi wa shirika linalojihusisha na maendeleo ya afya katika jamii nchini, Dkt.Patrick Mugasa amesema shirika lake limeendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali yaifikie jamii kuhamasisha jamii kujitokeza kupima mara wanapohisi kukohoa makohozi yenye chembechembe za damu mara kwa mara pamoja na kuumwa.