Back to top

Idara ya Usalama yamkamata Rais wa Pakistani kwa tuhuma za rushwa.

11 June 2019
Share


Rais wa zamani wa Pakistani, Asif Ali Zardari,amekamatwa na maafisa wa idara ya usalama kwa tuhuma za rushwa, hatua ambayo ni pigo kwa chama cha upinzani nchini humo cha Pakistan People's Party,(PPP).

Msemaji wa idara ya uwajibikaji ya taifa,NAB,Nawazishi Ali, amethibitisha kukamatwa kwa Zardari lakini hakutoa maelezo ya ziada.

Vyombo vya habari nchini Pakistan vimesema idara ya NAB imemkamata Zardari kutokana na uchunguzi kuhusu akaunti bandia za benki na utakatishaji wa fedha.