Back to top

IDRISS DEBY KUWANIA URAIS CHAD

25 March 2024
Share

Baraza la Kikatiba nchini Chad limepitisha majina 10 ya wagombea watakaowania nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao, ambapo miongoni mwao ni Rais wa Mpito wa Taifa hilo Jenerali Mahamat Idriss Deby, ambapo uchaguzi wa Urais nchini Chad umepangwa kufanyika Mei 6 mwaka huu, ikiwa ni moja ya jitihada za kurejesha utawala wa Kidemokrasia nchini humo.

Alipochukua madaraka mwaka 2021 kufuatia kifo cha Baba yake Idriss Deby Itno, Jenerali Mahamat aliahidi kufanyika kwa uchaguzi na kurejeshwa kwa utawala wa kidemokrasia ndani ya kipindi cha miezi 18.

Hata hivyo aliahirisha uchaguzi huo mpaka mwaka huu wa 2024, hali iliyozusha maandamano katika maeneo mbalimbali ya Chad.

Miongoni mwa wagombea kumi wa Urais nchini Chad, yumo kiongozi wa upinzani nchini humo Succès Masra ambaye mwezi Januari mwaka huu aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Mpito ya Chad.