Back to top

IGP Sirro akagua mafunzo ya utayari Kilelepori

09 April 2018
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, leo amekagua mafunzo ya utayari yakuwajengea uwezo askari wa Jeshi hilo yanayoendelea kufanyika Kilelepori wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Ambapo pia IGP Sirro amekagua ujenzi wa upanuzi wa madarasa na mabweni katika Chuo cha Polisi Moshi, yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua Zaidi ya wanafunzi 800 ambapo kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 60 ujenzi unaofanywa kwa msaada wa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.

Kwa upande wake kamishna wa Polisi Jamii CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa mafunzo ya kuwajengea uwezo askari yanayoendelea kilelepori ni muendelezo wa mkakati wa Jeshi la Polisi kuhakikisha linakuwa na askari wenye weledi wakati wanapotimiza majukumu yao ya kazi za Polisi.