
Rais wa Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF), amekitunuku tuzo ya Ariel Heart of Gold, Kituo cha runinga cha ITV, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa kituo hiki katika kuandaa maudhui yanayohusu utoaji wa elimu juu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu na Virusi Vya Ukimwi hapa nchini.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo yenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, Bi. Yolanda Brignoni (wa pili kutoka kulia), ambaye aliambatana na Mwakilishi Mkazi wa EGPAF Tanzania, Dkt. Sajida Kimambo (wa kwanza kulia) na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Joyce Mhaville (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko ITV, Joyce Luhanga (wa kwanza kushoto).
