Back to top

JENGENI STENDI ZA MABASI ZENYE UBORA

17 September 2023
Share

Serikali imezitaka idara zinazohusika na ujenzi katika Halmashauri kuhakikisha zinajenga stendi za mabasi zenye ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa.
.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, wakati akizindua mradi wa ujenzi wa Stendi ya kisasa ya magari katika Kijiji cha Lundusi, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, unaotekelezwa na Ofisi ya Rais kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
.
Aidha, Mhe.Mhagama, amesema kuwa hawatarajii eneo la manunuzi ya ujenzi likawa ni kichaka cha upotevu wa fedha.