Back to top

JESHI LA POLISI LAINGIA MAKUBALIANO NA TIA

15 September 2023
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura amesema Jeshi hilo limewekeza zaidi katika kufanya utafiti, elimu na mafunzo ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa jamii na Kwenda mabadiliko ya dunia ya sasa.

IGP Wambura amesema hayo wakati aliposhirikia hafla ya utiaji Saini, Hati ya Makubaliano na Mashirikiano baina ya Jeshi la Polisi Tanzania, kupitia Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam,na Taasisi ya uhasibu Tanzania, ambapo ushirikiano huo utawesha Jeshi hilo kujiendeleza kitaaluma hasa eneo la mafunzo na tafiti mbalimbali.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo amesema kuwa, Jeshi la Polisi liataendelea kufaidi mashirikiano yaliyopo kati ya Chuo cha Uhasibu Tanzania huku akibainisha kuwa changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii zitapatiwa ufumbuzi kutokana na mashirikiano walioingia na Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es salaam  Dkt. Lazaro Mambosasa, amesema kuwa mashirikiano kati ya Jeshi la Polisi, kupitia Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, na na Taasisi ya Uhasibu Tanzania, ni ya awali ambayo yamejikita zaidi kwenye eneo la usalama na kitaaluma.