
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dkt. Paul Lawala ametoa wito kwa vyuo vyote nchini kuwa mabalozi wa utambuzi wa msingi juu ya afya ya afya ya akali ili kusaidia kuwa na wananchi wenye ustawi wa afya ya akili
Dkt. Lawala ametoa rai hiyo leo Mkoani Iringa wakati akizungumza na Wanafunzi wa Vyuo vikuu vya Iringa na Ruhaha katika Kampeni ya Kitaifa ya afya ya akili ni Afya
“Tunahitaji vyuo hivi kuwa sehemu ya kusaidia jamii kuwa na uelewa juu ya afya ya akili ili kulinda taifa na kuinua uchumi wa taifa letu kwa kuhakikisha kila mtanzania anaustawi wa afya ya akili”, ameeleza Dkt. Lawala
Amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kujenga uelewa vitu gani vinasababisha na kuhitajika kutunza afya ya akili ya mtu ambapo amesema kuwa ubalozi huo ufanyike ndani ya vyuo vyao hadi nje ya vyuo na maeneo jirani ili kusaidia jamii kuwa na uelewa mzuri juu ya ustawi wa afya ya akili
Amesema kuwa anaimani mpka baada ya miaka mitatu ya kampeni hiyo kuwa imekamilika wananchi wengi watakuwa wameongeza uelewa zaidi juu ya afya ya akili na uwezo wa mtu binafsi kutambua uwezo wake utakuwa umeongezeka
Kwa upande wake Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Dina Kisambi amesema kuwa jamii kubwa ya watanzania bado hawana uelewa wa kutosha juu ya afya ya akili hivyo ujio wa Kampeni hiyo itasadia kuongeza kasi ya uelewa juu ya ustawi wa afya ya akili.
Amesema kuwa atahakikisha kwamba wanakuwa mabalozi wazuri kwa wengine ili kuongeza uelewa juu ya afya ya akili .
“ Aidha amemshukuru kwa Chuo Kikuu Iringa kwa kutunukiwa tuzo ya utambuzi kama wadau wa afya ya akili kwani wao pia ni wazalishaji wazuri wa wataalamu wa saikolojia na afya ya akili