
Rais wa Rwanda, Mhe.Paul Kagame amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania na kurejea nchini Rwanda ambapo ameagwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Stergomena Tax ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar, Mhe.Jamal Kassim Ali na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye.
