Back to top

Kajala, Rayvanny wahojiwa sakata la picha za utupu za Harmonize.

20 April 2021
Share

Jeshi la Polisi Kanda Kaalum limesema limemkamata msanii Frida Kajala,Paula Paul, Raymond Shaban Mwakyusa (Rayvanny) Clayton Revocatus (baba Levo) na wengine wawili kwa mahojiano kufuatia sakata la kusambaa picha za utupu za msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu (Harmonize) na watu hao wameachiwa kwa dhamana.


Kamanda Mambosasa amesema hatua hiyo imekuja baada ya Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu (Harmonize) kutoa malalamiko hayo.

Watuhumiwa hao wote wameachiwa kwa dhamana baada ya kumaliza kuhojiwa na uchunguzi wa kesi hiyo bado unaendelea.