Back to top

KIBOKO NA SIMBA WALIOZUA TAHARUKI, WADHIBITIWA

09 March 2023
Share

Askari wa Wanyamapori, wa Mamlaka ya Udhibiti wa Wanyamapori nchini (TAWA), mkoani Ruvuma wamefanikiwa kuwadhibiti wanyama aina ya kiboko na simba walioingia kwenye makazi ya wananchi na kusababisha hofu na taharuki, kwa wakazi wa Kigosera na Mpepayu wilayani Mbinga, baada ya wanyama hao kuua mifugo na kuharibu mazao.