Tume ya vyuo vikuu nchini imevifutia usajili vyuo vikuu vitatu kikiwemo chuo kikuu cha kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU).
Akizungumza na wanahabari Katibu Mtendaji wa (TCU) Prof.Charles Kihampa amesema wamelazimika kuvifuta vyuo hivyo baada ya kujiridhisha kuwa hata wakiongezewa muda hawatakidhi vigezo.
Aidha amesema wameridhia wamiliki wa vyuo vikuu vishiriki viwili na vituo vitatu vya vyuo vikuu kusitisha utoaji wa mafunzo baada ya kuona kwamba hawawezi kuendana ana hali halisi.
Aidha tume hiyo imeridhishwa na maboresho yaliyofanyw ana chuo kikuu kishiriki cha afya na sayansi shirikishi cha mtakatifu Francisco kwa kurekebisha mapungufu waloiyokuwa nayao hivyo tume imekiruhusu kuanza kudahili wanafunzi wapya kuanzia mwaka wa masomo 2020/2021.