
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo ameileza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuanzisha kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida za Muungano.
Dkt.Jafo amesema Mungano wa Tanganyika na Zanzibar umeendelea kuimarika kutokana na upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi na hivyo kuufanya uwe wa kipekee duniani.
Amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Kamati hiyo.
Amesema Serikali itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Pamoja na yale masuala 22 ya Muungano kwa mujibu wa Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika ipasavyo.
