
Serikali mkoani Njombe imetekeleza agizo la Rais Dkt.John Magufuli la kuanza kutumia kituo kipya cha mabasi ndani ya siku 30 tangu Aprili 10 2019 ambapo ujenzi wa kituo hicho ulionekana kutumia muda mrefu.
Mapema Leo Mei 11 vyombo vya usafiri vya mkoa huo vimeanza kutumia kituo hicho kipya kama agizo la mkurugenzi Wa halmashaur ya mji wa Njombe lilivyoarifu hapo Mei 9 2019 la kuwataka wasafirishaji kuhamia katika kituo hicho.