Back to top

KOCHA WA TAIFA STARS KULIPWA NA SERIKALI

07 March 2023
Share

Serikali imesema itamlipa mshahara Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Adel Amrouche ambaye ni Raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria, ambapo imebainisha kuwa hatua hiyo ni katika kuendeleza mchezo wa soka hapa nchini.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, wakati wa kumtambulisha Kocha huyo kwenye Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.