
Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala, amesema ili kuwezesha watoto wakike kupata taulo kwa ajili ya kujisitiri, LSF imeandaa mbio za 'Run For Binti Marathon 2023'ikiwa ni mkakati wa kukusanya rasilimali fedha, ili kuwezesha watoto wakike kupata taulo na kuboresha upatikanaji wa haki ya afya ya uzazi, hususani hedhi salama na safi.
Amesema licha ya kumpatia pia binti taulo za kike lakini pia ni pamoja na kumboreshea mazingira bora na rafiki katika sekta ya elimu kwa mtoto wa kike yatakayomuwezesha kupata hedhi salama kupitia ujenzi wa miundombinu bora hususani vyoo.



Ameeleza hayo mkoani Dar es Salaam, wakati akiingia ubia na Smile for Community Organization (S4C).
