Back to top

LSF YAMULIKA WANAWAKE ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI, LONGIDO.

31 January 2023
Share

Wanawake na wasichana wa wajamii ya Kimasai takribani 2500 wilayani Longido, wanategemea kunufaika kupitia mradi wa miaka miwili uliolenga kuinyanyua jamii hiyo kiuchumi na kielimu.
 
Akiongea kuhusiana na mradi huo ambao utatambulika kwa jina la "Wanawake Tunaweza" unafadhiliwa na Legal Services Facility (LSF) na wadau wa wamaendeleo, Luxembourg, Mkurugenzi Mtendaji (LSF) Lulu Ng'wanakilala amesema mradi huo utatekelezwa Wilaya Longido mkoani Arusha, ilikuwawezesha wanawake na wasichana wa jamii ya kimasai katika mkoa huo kwa kuwasaidia kuunda vikundi vya kiuchumi na kuwajengea uwezo wakibiashara na ujasiriamali ikiwemo kuwapatia masoko na upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kike kwa kuhakisha wanawajengea  mabweni.

Aidha Ng'wanakilala ameongezea kuwa kutokana na jamii ya kimasai kudumisha mila na desturi kwa muda mrefu ambapo asilimia 85 ya uchumi wao hutegemea mifugo, huku shughuli zote hizo ikiwemo uzalishaji mali milikiwa na kundeshwa na wanaume suala ambalo linapelekea haki za wanawake na wa sichana kukiukwa kupitia mradi huo utatatua baadhi ya changamoto kwenye jamii hiyo.

Kwa upande wamwakilishi wa mgeni rasmi katibu tawala wa longido hassan ngoma amesema ujenzi wa mabweni ya watoto wa kike katika shule za sekondari za lekule na namanga utawezesha kutatua changamoto ya watoto kubanana kwenye bweni moja na kuongeza idadi ya watoto wa shule shuleni