Back to top

LSF YATATUA MIGOGORO 175 KWA NJIA YA USULUHISHI

30 January 2023
Share

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF) Bi.Lulu Ng'wanakilala amesema kwenye wiki ya sheria 2023, migogoro 175, mirathi, migogoro ya wanandoa na watoto kutopewa matunzo, imefanikiwa kutatuliwa kwa njia ya usuluhishi, ambapo wanaume ni 73 na wanawake ni 102. 

Bi. Ng'wanakilala amesema amesema wameamua kuweka mkazo kwenye usuluhishi, ilikwenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka 2023, inayosema 'Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu'. 

Kwa upande wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Usuluhishi, Jaji Dt.Zainab Mangualuo, Mahakama kwa sasa zinaendelea kukabiliwa na mashauri mengi, ambayo yanahitaji ushahidi ilikufanya maamuzi ya mwisho suala ambalo huchukua muda mrefu, tofauti na usuluhishi ambao huchukua siku 30.