Back to top

Lukuvi aagiza matapeli 5 vinara migogoro ya ardhi Mapinga kukamatwa.

20 July 2021
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi ameamuru kukamatwa watu watano akiwemo Katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mapinga Omar Shaaban na kuliagiza Jeshi la Polisi kuwafanyia mahojiano kwa tuhuma za kuhusika na utapeli wa kuuza ardhi za wananchi kiholela na kusababisha migogoro mingi katika kata hiyo.

Akiamuru kukamatwa kwa watu hao katika operesheni yake endelevu ya ondoa migogoro ya ardhi mkoani Pwani katika mkutano wa wananchi eneo la Mapinga licha ya kupewa orodha ya watu 54 wanaojihusishaa na matukio hayo aliiagiza serikali mkoani Pwani kila wilaya iwe na daftari la migogoro yaa rdhi ili iundwe tume kushughulikia migogoro.

Naye Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar kunenge alieleza kukithiri kwa migogoro ya ardhi ndani ya mkoa wake huku baadhi ya viongozi kata ya Mapinga wakaeleza ushiriki wa badhi ya viongozi wenzao wa CCM kuuza na kuchochea migogoro ya ardhi Mapinga.

Katika ziara hiyo pia Mhe.Lukuvi alizungumza na wananchi wa Makurunge na kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya mwekezaji kampuni ya Genenter na Green Wuud anayemiliki ekari zaidi ya 1000 kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu na kuababisha wananchi kuvamia na kuibuka kwa mgogoro huo.