Back to top

Madaktari 2 kutoka Cuba watekwa nyara na Al-Shabab Mandera Kenya.

12 April 2019
Share

Madaktari wawili kutoka nchini Cuba waliotumwa kufanya kazi kwenye Kaunti ya Mandera kilomita 810 kutoka jijini Nairobi wametekwa nyara na washukiwa wa Al-Shabab katika mji wa mpakani wa Mandera.

Mmoja kati ya walinzi wa madaktari hao ameuwawa huku mmoja akifanikiwa kutoroka.

Vikosi vya usalama vinawasaka wanamgambo hao ambao walijaribu kutorokea taifa jirani la Somalia.