Back to top

Magunia 100 ya mahindi yatolewa kwa ajili ya chakula cha wanafunzi.

13 July 2021
Share

Mbunge wa Jimbo la Mbozi, Mhe.George Mwenisongole ametoa Magunia 100 ya mahindi na mengine 20 ya Mchele vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Shilingi Million 5.88 kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa kidato 4 walioweka kambi mashuleni wakijiandaa na mitihani ya kuhitimu.

Pia mbunge huyo ametoa zawadi ya Shilingi 200,000 kwa kila Mwanafunzi aliyepata ufaulu wa daraja la kwanza (DIV. I) kwa wahitimu 25 wa mitihani ya kidato cha 4 kwa mwaka 2020, kutoka Shule zote za sekondari za Jimbo la Mbozi.