
Mahakama Kuu ya Tanzania, imetupilia mbali shauri la Humphrey Malenga, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali la kupinga uamuzi wa Rais kumwongezea muda, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Juma.
Katika hukumu hiyo Mahakama Kuu imesema kitendo cha Rais kumwongezea muda Jaji Mkuu hakikuwa kinyume cha katiba kwa sababu mamlaka ya Rais, kumwongezea muda Jaji Mkuu yalikuwa sahihi kwa mujibu wa Ibara 120 kifungu cha pili, tatu na nne.
Mahakama imesema Ibara 118 haiwezi kusimama yenyewe kwa sababu inafanya marejeo katika Ibara 120, kifungu cha kwanza inayosomwa pamoja na Ibara ya 120 kifungu cha pili na cha tatu.
Aidha Mahakama kuu imesema Jaji Mkuu ana sifa, kama Majaji wengine wa Mahakama ya rufani hivyo hawezi kutenganishwa.