Back to top

MAJALIWA AFUNGUA KOZI FUPI YA 13 YA VIONGOZI.

02 August 2022
Share

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa amewataka washiriki wa kozi fupi ya 13 ya viongozi, watambue, wafuate na waisimamie falsafa ya Serikali iliyojielekeza katika kuwahudumia Watanzania.

Mhe.Majaliwa amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya ulinzi na Stratejia kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatarajia kuona mabadi liko ya mtazamo, ushauri na uamuzi watakaoufanya unapaswa kuakisi walichokipata kupitia kozi hiyo baada ya viongozi hao kurudi kwenye maeneo yao ya utendaji.

Ametoa kauli hiyo leo alipofungua kozi fupi ya 13 ya viongozi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Dar Es Salaam.

Kozi hiyo inahudhuriwa na baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Waandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Taasisi za Kimkakati za Serikali.