Makamu wa Rais apiga marufuku wakulima wa mpunga kutozwa kodi shambani


Makamu wa Rais mh. Samia Suluhu Hassani amepiga marufuku tabia ya halmashauri ya wilaya ya Moshi kuendelea kuwatoza wakulima wa mpunga ushuru wa mazao  mashambani  msimu wa mavuno. 
 
Makamu wa Rais ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kwa wakulima wa mpunga kata ya Mabogini  skimu  ya umwagiliaji Lower Moshi kutozwa kodi mashambani kabla ya kutoa mazao shambani.