Back to top

MALIJENDI WA RIADHA KATIKA PICHA YA PAMOJA

20 April 2024
Share

Malijendi wa Riadha Filbert Bayi Sanka, Juma Ikangaa na Suleimani Nyambui wamekutana katika Twende Olimpic Paris 2024 jijini Dar es Salaam.

Filbert Bayi Sanka mwaka 1974 aliweka rekodi ya dunia ya mbio za Mita 1500 iliyodumu mpaka mwaka 2022, ana medali ya fedha ya Olimpic ya Mita 3000 aliyoichukua Moscow mwaka 1980 ni alama kubwa ya mchezo wa Riadha, ana medali mbili za dhahabu za All Africa Games 1973 na 1974. 

Juma Ikangaa Mtanzania aliyebeba medali mbili mwaka mmoja mshindi wa medali ya dhahabu All Africa Games mwaka 1982 na Mshindi wa medali ya fedha Brisbane Australia 1982 katika mashindano ya Jumuiya ya madola.

Ikangaa ni mfalame wa marathon, ana medali za dhahabu 7 katika mbio za Tokyo Marathon ( Japan), Melbourne Marathon (Australia), Beijing Marathon (China), New York Marathon (Marekani). 

Suleimani Nyambui Mshindi wa medali ya fedha mbio za Mita 5000 mwaka 1980  akimaliza nyuma ya mwanariadha hatari wa Ethiopia Miruts Yifter, All Africa Games mwaka 1978 akalipa heshima Taifa Kwa medali ya shaba.

Nyambui ni mshindi wa kwanza mara mbili mfululizo Berlin Marathon mwaka 1987 na 1988.Na mwaka huo 1988 alishika wa kwanza kwenye Stockholm Marathon.