Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, imeongoza katika ukusanyaji wa mapato, ambapo imekusanya asilimia 247 ya makisio yake ya mwaka, ikifuatiwa na Halmashauri za Wilaya ya Mlele 185%, na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro 158% , huku Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli ikiwa ya mwisho kwa kukusanya 58% ya makisio yake ya mwaka, ikifuatiwa na Halmashauri za Wilaya ya Korogwe 67% na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda 70%.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa TAMISEMI, Mhe.Innocent Bashungwa , wakati akitoa taarifa kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo amebainisha kuwa Halmashauri 100 zimekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 100 au zaidi ya lengo la mwaka.