Back to top

MAREKEBISHO BANDO NA VIFURUSHI VISUBIRI KAULI YA SERIKALI

23 November 2022
Share

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imewataka watoa huduma za mawasiliano nchini kutofanya marekebisho yeyote ya bei za bando mpaka serikali itakapomaliza kufanya tathimini na mapitio ya gharama halisi juu ya bei elekezi ya bando na vifurushi kwa watoa huduma hao.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye na  amesema kufikia mwezi ujao, tathimini hiyo ya gharama halisi juu ya bei elekezi itakamilika.

Aidha Waziri Nape amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati, serikali ikipitia tathimini hiyo itakayokuja na mapendekezo ili  kukomesha upandishaji holela wa garama za bando na vifurushi kwa watoha huduma hao.