
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imepiga marufuku matumizi ya rangi za upinde wa mvua (Rainbow) mashuleni ,huku ikizataka shule zote kuacha kuagiza vitabu nje ya nchi, mpaka vitakapothibitishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.
.
Marufuku hiyo imetolewa na Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Lela Muhamed Mussa, ambapo pia amebainisha kuwa ,shule ya Msingi ya Seed of Life iliyokuwa ikidaiwa kuhusika na vitendo vinavyokiuka maadili, imechunguzwa na kubainika kuwa haihusiki na vitendo hivyo.
