Back to top

"MASHINDANO YA SILAHA ZA NYUKLIA NI WENDAWAZIMU"-GUTERRES

28 September 2023
Share

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres, ameonya kuhusu dunia kuingia katika mashindano mapya ya silaha za nyuklia ambayo yanaweza kueneza maafa duniani kote.

Guterres amesema mashindano ya silaha yanatia wasiwasi wa kuongezeka karibuni idadi ya silaha za nyuklia ulimwenguni.

Bwana Guterres ameyaita mashindano mapya ya silaha za nyuklia duniani kama ya kiwendawazimu, amesema matumizi yoyote ya silaha za nyuklia, wakati wowote, mahali popote na katika mazingira yoyote, yatasababisha maafa ya kibinadamu na kusisitiza kuwa lazima siasa na mwenendo huo ubadilike.

Ametoa wito kwa nchi zote duniani zizingatie hilo na zisijitumbukize kwenye janga la maafa ya nyuklia.