
Mchezaji timu ya ligi ya Ujerumani, Schalke 04, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rabbi Matondo amesema amekuwa muathirika wa matusi ya kibaguzi kwenye mtandao wa Instagram.
Matondo ambae anacheza nafasi ya ushambuliaji wa pembeni katika timu hiyo amesambaza picha ya ujumbe wa kibaguzi katika ukurasa wake wa Twitter, akisema jukwaa hilo halijafanya lolote kuhusu ubaguzi wa rangi.