
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa CHADEMA BAWATA na Mbunge wa Kawe Mh.Halima Mdee amekamatwa alipowasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea Afrika Kusini na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam.
Kamanda wa wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Bw.Lazaro Mambosasa amekiri kumshikilia Halima Mdee na kwamba anaohojiwa na kisha atafikishwa mahakamani peke yake kwa sababu wengine walikwishasomewa mashtaka yao.
Mkurugenzi wa itifaki,mawasiliano na mambo ya nje wa CHADEMA Bw. John Mrema amesema Halima ni mgonjwa na amerejea nchini akitoka kwenye matibabu Afrika Kusini jambo ambalo kamanda mambo sasa amesema hawawezi kuthibitisha kwa kuwa suala la ugonjwa linahibitishwa na daktari.
Mh.Halima Mdee ni miongoni mwa viongozi wakuu wa CHADEMA waliokuwa wanatakiwa kuripoti polisi kujibu tuhuma zinazowakabili.Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman mbowe na wenzake watano wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yao .