
Mbwa wa miguu sita aliyetelekezwa katika kituo cha magari cha maduka makubwa, huko Wales, amefanyiwa upasuaji wa kuondoa miguu yake vya ziada.
Ariel, spaniel, alizaliwa na kasoro nyingi za kiafya na alipewa jina la binti wa kifalme wa Disney, kwa sababu miguu yake ya ziada ya nyuma iliyokuwa imeungana kwa kiasi, ikifanana na mkia wa nguva.
Mbwa huyo Alichukuliwa na Greenacres Rescue, kikundi cha kujitolea, kilichopo katika mji wa Haverfordwest huko Pembrokeshire, Wales na kilisimamia upasuaji wa Ariel na kumtafutia familia ya kulea.
Amba mbwa huyo (Ariel) sasa amepata nafuu na anatembea kawaida.
