Back to top

Mfumo wa usambazaji wa vifaa vya TEHAMA mashuleni watakiwa kuimarishwa

01 August 2021
Share

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew ameitaka Taasisi ya Mawasiliano ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuimarisha na kusimamia ipasavyo taratibu za manunuzi na usambazaji wa vifaa vya TEHAMA mashuleni ili kuhakikisha kinachotarajiwa kufika katika shule husika kinafika bila mapungufu yeyote.

Mhandisi Kundo ameyasema hayo alipotembelea Shule ya Sekondari Mabira iliyopo katika Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera kwa ajili ya kukagua chumba cha kompyuta cha shule hiyo kilichowezeshwa vifaa vya TEHAMA na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kukuta kuna vifaa vingine vya TEHAMA vilivyopelekwa katika shule hiyo kwa ufadhili wa UCSAF ambapo Mkuu wa shule hiyo Bw. Danford Nuvia akithibitisha kupokea kompyuta nne na printa moja tofauti na utaratibu wa Mfuko huo wa kupeleka kompyuta tano na printa moja katika miradi yake ya kusambaza vifaa vya TEHAMA katika shule za msingi na sekondari nchini.