Back to top

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAONGEZEKA

09 February 2023
Share

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2023, umeongezeka kutoka 4.8% kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2022, hadi  4.9%, ambapo imebainisha kuwa, kuongezeka kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Januari 2023, ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Disemba 2022.